Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Wanafunzi wafichua siri wanaowalawiti

20th May 2012
Print
Comments
  Wahusisha wazazi, walezi majumbani
  Ni baada ya kampeni ya `watoto tuache tuseme`

Tukio la Wanafunzi kufanya vitendo vya kulawatiana katika Shule za Msingi Yombo Buza jijini Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya kubainika baadhi ya wazazi na walezi wanahusika kwa kuwafanyia vitendo hivyo watoto wao majumbani.

Kubainika kwa hali hiyo kumekuja baada ya uongozi wa Manispaa ya Temeke kuanzisha kampeni maalum inayoitwa 'Watoto tuache tuseme' inayohusisha shule 10, ambapo watoto hao wanapata nafasi ya kuelezea matatizo mbalimbali yanayowapata au kuyaona ndani ya jamii.

Akizungumzia suala hilo, Afisa Elimu Kilimo, Saveria Kannole, ambaye pia ni Mratibu wa kampeni hiyo, alisema watoto hao wamefichua siri hiyo baada ya kutakiwa kuandika ujumbe kwenye karatasi unaozungumzia maisha yao pamoja na matatizo ndani ya shule yao.

Alisema kutokana na kupewa nafasi hiyo wanafunzi hao walieleza matatizo yao mbalimbali na baadhi yao walifichua kuwa baadhi ya wazazi wanawalawiti wanaporudi majumbani kwao na kuomba wapewe matibabu.

Alisema kampeni hiyo ya watoto tuache tuseme imepelekwa shuleni hapo mara baada ya kutokea matukio ya wanafunzi kulawitiana kwenye shule hiyo kama njia ya kuongeza uelewa wa kujifahamu na kutambua thamani yao miongoni mwa wanafunzi hao.

"Tumegundua na kubaini chanzo cha wale watoto mpaka kufikia hatua ya kulawitiana na kuvuta bangi inatokana na baadhi ya wazazi kutowajibika katika malezi na wengine kuhusika kuwafanyia watoto wao vitendo hivyo vya kinyama," alisema Kannole.

Alisema imekuwa vigumu kuwakamata wazazi wenye tabia hiyo kutokana na ujumbe walioandika watoto hao kutokuwa na majina wala anuani zao za kuwatambulisha.

"Kuna mmoja alifichua kuwa akirudi nyumbani mjomba wake anamfanyia vitendo hivyo, lakini tulishindwa kumpata baada ya wanafunzi wenzake kutokuwa tayari kumtaja," alisema.

Alisema kimsingi hawajachukua hatua ya kuwafukuza shule watoto waliotajwa na wenzao kwamba wanajihusisha na tabia hiyo kutokana na kupingana na sheria ya haki za watoto.

Kannole alisema kitu walichokifanya ni kuhakikisha wanaunda timu maalumu ya kubadilisha mienendo ya watoto hao pamoja na kuwapa uwezo wa kuongea mara wanapoona kuna tatizo.

Mafanikio yanayopatikana katika mpango huo ni pamoja na watoto ambao hawawezi kujirekebisha kuamua kuacha shule wao wenyewe baada ya kuona wanafunzi wote wamekuwa wazi kwa kuripoti kwa walimu kila kitu wanachokiona.

Afisa Elimu huyo alisema kampeni hiyo iliyoanza kwa shule 10 ndani ya Manispaa inafadhiliwa na Shirika la watoto Duniani (Unicef) ambapo inahusisha shule za msingi Temeke, Bahati, Wailes, Likwati, Nzasa, Chemchem, Charambe, Kilamba, Chekeni mwasonga na Vumulia ukooni.

Alieleza kuwa katika shule hizo zilizoanza na mpango huo hakuna kesi zinazohusiana na vitendo viovu kwa wanafunzi kutokana na matukio mengi kabla ya kufanyika kujulikana na kudhibitiwa na walimu.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles