Monday May 2, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Nchunga awapuuza wazee

24th May 2012
Print
Comments
Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga

Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, ameonekana kupuuzia "kelele" zinazopigwa na baadhi ya wanachama wanaoongozwa na Baraza la Wazee la klabu hiyo wanaomtaka ajiuzulu kwa kuendelea kuchapa kazi.

Nchunga aliiambia NIPASHE kwamba wamepokea maombi ya makocha watano wa kigeni wanaotaka kuziba nafasi iliyoachwa na Mserbia Kostadin Papic.

Hata hivyo, alisema kuwa Kamati ya Utendaji inashindwa kukutana kujadili masuala ya maendeleo na badala yake inatumia muda mrefu kupanga njia za kumaliza mgogoro uliopo.

Nchunga bila kutaka majina ya makocha hao waliotuma maombi alisema kuwa wawili kati yao wanatoka Serbia huku wengine ni kutoka Uholanzi, Ureno na Scotland.

"Ni ngumu kufanya maamuzi katika hali tuliyonayo, hata zoezi la usajili pia linasuasua na litakuwa gumu safari hii, hali hii inatuumiza na hatma yake itakuwa si nzuri hapo baadaye," alisema Nchunga.

Aliongeza kuwa licha ya 'upepo mchafu' uliopo uongozi wake bado uko imara na wataendelea kufanya kazi kama katiba inavyoeleza huku hivi sasa wakifanya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa wanachama unaotarajiwa kufanyika Julai 15 hapa jijini Dar es Salaam.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles