Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Wanawake CCM waibana Serikali idhibiti mfumuko wa bei

21st May 2012
Print
Comments

Serikali imetakiwa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na mfumuko wa bei uliopo kama ilivyoagizwa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC-CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya CCM, Amina Makilagi, alisema umoja huo unapongeza uamuzi huo wa Nec.

Makilagi alisema mbali na serikali kuchukua hatua za haraka lakini pia iendelee na mipango yake ya muda mrefu ya kukabilia na tatizo hilo la mfumuko wa bei za bidhaa hasa za vyakula.

Alifafanua kuwa maamuzi ya  NEC kuiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka na muda mfupi ikiwamo kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula na ya ongezeko la thamani (VAT) katika sukari itasaidia kupunguza mfumuko wa bei na kuwaondolea mzigo wa gharama za maisha Watanzania.

Aliiomba Serikali kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni hasa katika hoteli na maduka mengine yanayotoa huduma kwa wananchi na kuwahimiza  waajiri wahimizwe kupandisha mishahara na malipo mengineyo kwa wafanyakazi.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles