Wednesday Jun 19, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Jenerali Kiaro kuzikwa Tarime Jumamosi

12th April 2012
Print
Comments
Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali, Ernest Kiaro

Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali, Ernest Kiaro, anatarajiwa kuzikwa Jumamosi nyumbani kwake mjini Tarime Mjini Mkoa wa Mara.

Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Kapambala Mgawe, alisema marehemu Kiaro anatarajiwa kuzikwa keshokutwa na taratibu za kuuaga mwili zitaanza saa sita mchana mpaka saa tisa alasiri.

Hata hivyo, alisema mgeni rasmi kutoka serikalini bado hajafahamika.

Nacho Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia Kurugenzi ya Habari kimetoa salamu za rambirambi kwa kusema kimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Jenerali Kiaro.

Katika slamu hizo kimewapa pole  ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Jenerali Kiaro, ambaye alifariki dunia juzi asubuhi wakati akipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bigando jijini Mwanza.

“Chadema kwa majonzi makubwa kinatuma salaam za pole na rambirambi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, kwa niaba ya Majeshi ya Ulinzi kwa kumpoteza mmoja wa wapiganaji shupavu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza:

“Chama kinatuma salaam za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki kwa msiba huo mkubwa.”

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment