Thursday Jun 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mafanikio bado udhibiti mapato Uwanja wa Taif

9th February 2013
Print
Maoni ya Katuni

Serikali, hivi karibuni, ilitoa utaratibu mpya wa ukakataji makato ya mapato yatokanayo na viingilio kwenye Uwanja wa Taifa ikiondoa rasmi tozo la asilimia 20, pamoja na makato mengine.

Serikali ambayo ilikuwa ikichukua asilimia 10 ya mapato kwenye uwanja huo kwa 'huruma' kutoka kiwango halisi hicho cha asilimia 20, iliamua kuwa itachukua asilimia 15 na kuondoa mlolongo wa makato mengine, mengi yakiwa yenye kufanana, ili kuota ahueni kwa timu ambazo zitautumia.

Lakini kama ambavyo viongozi wa klabu kubwa za Simba na Yanga wamewahi kusema baada ya michezo ya duru la pili la ligi kuu ya Bara tangu kupitishwa kwa uamuzi huo mwezi uliopita, nia ya serikali haijafanikiwa kutokana pamoja na mambo mengine, tunaona Nipashe, kuongezeka kwa gharama za kipengele cha uchapaji tiketi hasa kwa mechi ambazo si za ligi kuu ya Bara.

Katika mechi za ligi kuu ya Bara, ambako pia kuna wasiwasi kuwa kiwango halisi kilipaswa kuwa chini ya gharama ambazo hutolewa rasmi na shirikisho la soka, TFF, wastani wa fedha za uchapaji tiketi kwa mchezo mmoja huwa ni sh. milioni 3.5 hivi.

Lakini katika michezo miwili ya kirafiki kati ya timu mbili kuwa za Bara -- Yanga na Simba -- dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini mwezi uliopita, kwa mfano, tumegundua Nipashe, tiketi za michezo hiyo kwenye Uwanja wa Taifa ziligharimu sh. milioni 15 kwa kila mechi.

Ingawa hapakuwa na malalamiko kutoka kwa viongozi wa Yanga na Simba wasioridhishwa na fungu la sh. milioni 3.5 kwenye ligi, katika michezo hiyo ambayo zilikaribishwa, kwa vyovyote, kiasi cha sh. milioni 15 kuwa gharama za uchapaji tiketi katika mchezo ambao unafanyika kwenye uwanja ambao una utamaduni wa kuchapa tiketi kwa gharama nafuu hakipaswi kukubaliwa na timu husika, Nipashe tunaona. 

Na katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Taifa Stars na Cameroon katikati ya wiki, mchanganuo wa makato ya mapato unaonyesha kuwa gharama za uchapaji tiketi katika mchezo ambao uliingiza sh. milioni 148 zilikuwa ni sh. milioni 7.3.

Kiasi cha sh. milioni 7.3 katika uchapaji tiketi kutoka katika fungu la sh. milioni 148, na kwa kulingnaisha na sh. milioni 15 za michezo iliyokwisha tajwa, kinaweza kuonekana kuwa ni kidogo hasa kutokana na ukweli kuwa chapisho hufanyika kabla ya mchezo hivyo idadi maalumu ya watazamaji kuwa haijajulikana bado.

Na tunafahamu fika, Nipashe, kuwa kiasi hicho cha sh. milioni 7.3 kingeweza kuwa kidogo zaidi kimlingano kama idadi ya watazamaji waliojitokeza kulipia viingilio katika mchezo huo ingekuwa kubwa zaidi ya 23,000 ambayo haikutarajiwa na waandaaji.

Lakini bado tunaona kuwa kama TFF na waandaaji wa mechi kwenye Uwanja wa Taifa, kila mmoja kwa nafasi yake wangekuwa na moyo kama wa serikali, nafuu iliyotarajiwa kupatikana baada ya kitendo cha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ingeonekana.

Aidha, tunaona kuwa kama TFF na waandaaji binafsi wa mechi kwenye Uwanja wa Taifa, kila mmoja kwa nafasi yake wangekuwa na moyo kama wa serikali, nafuu iliyotarajiwa kupatikana baada ya kitendo cha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ingekuwa imeanza kunufaisha timu za taifa, klabu na wachezaji wetu kwa ujumla.

Manufaa hayo yangekuwa yameanza kuonekana kwa sababu katika pambano kati ya Stars na Camroon, kwa mfano, tena, gharama za uchapaji tiketi zilikuwa karibu nusu ya jumla ya bonafsi ambayo walipata wachezaji 23 na benchi la ufundi la Tanzania.

Ndiyo maana, tunasema Nipashe, mafanikio bado yapo mbali katika udhibiti wa mapato Uwanja wa Taifa.
 
   
   
 








 

SOURCE: NIPASHE