Wednesday Jun 19, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Airtel yatoa sare, viatu kwa wanafunzi shule ya Msingi Kiromo

11th February 2013
Print
Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki, akimvalisha sare za shule na viatu mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kiromo zilizotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel mwishoni mwa wiki hii.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imegawa sare za shule pamoja na  viatu katika Shule ya Msingi Kiromo iliyopo Bagamoyo, mkoani Pwani,  ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.

 
Shule hiyo ni moja kati ya shule zilizofaidika na mpango wa kampuni hiyo wa shule yetu na kuingiza kwenye ukarabati wa majengo na madarasa na kubadili mazingira ya shule ikiwamo kupatiwa vifaa vya kufundishia pamoja na kompyuta.
 
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja shughuli za kijamii wa Airtel, Hawa Bayumi, alisema kampuni hiyo imedhamiria kuendelea kusadia shule mbalimbali kwa kutoa vifaa ikiwapo vya kufundishia ili kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. 
 
“Tunaendelea kuboresha shule ya Kiromo kwa kutoa msaada wa unifomu na viatu kwa wanafunzi. msaada wa sare za shule tunaotoa ni pamoja na kaptula 600, sketi 600, mashati 1,193 na viatu 728, vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 50” alisema.
 
Alisema Airtel itaendelea kusaidia shule mbalimbali kwa kutoa vitabu na vifaa vya kufundishia, lengo likiwa ni likiwa kuzifikia shule nyingi zaidi katika mikoa yote ya Tanzania.
SOURCE: NIPASHE