Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Ahmed Msangi
Askari wa Jeshi la Polisi ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, jijini Dar es Salaam. Askari aliyeuawa ni mwenye namba G2641 Konstebo Mwinyijuma, ambaye alipigwa risasi kichwani na kufariki dunia papo hapo. Askari waliojeruhiwa ni namba F9922 Amelia, ambaye amejeruhiwa katika mguu wa kulia na mwingine namba G2461 Konstebo Jafari aliyejeruhiwa karibu na kiuno.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Ahmed Msangi, alithibitisha askari hao kupigwa risasi na majambazi hao.
Msangi, ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Kanda hiyo alisema askari waliojeruhiwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke na pia mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali hiyo. Alisema jana saa 7:00 mchana walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna kundi la majambazi wanataka kufanya uhalifu sehemu fulani. Msangi alisema kufuatia taarifa hizo, askari wa upelelezi walisambaa katika Jiji lote la Dar es Salaam kwa ajili ya doria ili kudhibiti uhalifu huo.
Alisema ilipofika saa 7:30 mchana, katika Barabara ya Nyerere, askari hao walilishuku gari dogo aina ya Toyota Carina lenye namba za usajili T319 BSY lililokuwa na vioo vya giza, ambalo lilipita kwa mwendo kasi likiwa na watu watatu.
Msangi alisema kutokana na hali hiyo, askari walianza kulifukuza kuanzia eneo la Jet Lumo. Alisema majambazi hao waliokuwa wakifukuzwa, walipofika katika mchepuo unaoelekea njia ya vumbi iitwayo “Mchichani”, Wilaya ya Temeke, ghafla walikutana na askari waliovalia sare za polisi wakiwa katika doria.
Alisema hali hiyo iliwafanya majambazi hao kupatwa na wasiwasi na kiwewe. “Mmoja wa majambazi alianza kufyatua risasi ovyo kuwaelekea askari hao na kuwajeruhi watatu,” alisema Msangi. Alisema baada ya tukio hilo, msako mkali ulianza, ambao uliwezesha kulikamata gari hilo na watu wasiopungua watano wanaoshikiliwa kwa uc