Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema atatoa ripoti kuhusiana vurugu zilizotokea katika hosteli za wanafunzi wa Chuo cha Usimsmizi wa Fedha (IFM) maeneo ya Kigamboni baada ya kurejea kutoka safarini.
Alisema ripoti hiyo iko tayari, lakini mpaka arejee kutoka safarini.
“Mimi niko safarini, hivyo nategemea kuitoa ripoti hiyo baada ya kurejea Dar es salaam, ripoti hiyo iko tayari na kila kitu kitaweka wazi baada ya hapo,” alisema.
Uongozi wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho (ISO) ulisema jana kuwa ulishataarifiwa kuwa Kova alikuwa safarini, hivyo mpaka atakaporejea ndipo watakaa pamoja na kutoa taarifa hiyo itakayotokana na uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo.
Waziri mkuu wa ISO, Daniel Sarungi, alisema kuwa licha ya wanafunzi wengine kuwa likizo, hakutazuia kutolewa kwa ripoti hiyo.
Wanafunzi wa chuo hicho wanoishi katika hosteli za Kigamboni waliandamana Januari 15, mwaka huu kupinga vitendo vya wenzao wkuporwa, kulawitiwa na kubakwa wanavyofanyiwa nabaadhi ya watu, hali iliyolilazimisha Jeshi la Polisi kuahidi kufanya uchunguzi na kutoa taarifa hadharani.