Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Ugawaji wa viwanja Mabwepande wazua vurugu

22nd May 2012
Print
Comments

Zoezi la uchukuaji fomu za ununuzi wa viwanja vipya vya Mabwepande, Mkoa wa Dar es Salaam, jana liligubikwa na vurugu, baada ya baadhi ya wananchi waliofika asubuhi kufuatilia fomu hizo kuanza kulalamikia uendeshwaji wake.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za ardhi, upimaji  na ramani za Manispaa ya Kinondoni, wananchi hao walisema zoezi hilo linaendeshwa katika mazimngira ya rushwa kutokana na baadhi ya watu kupatiwa fomu bila ya kufuata utaratibu wa foleni kwa kutanguliza vikaratasi vilivyoandikwa.

“Tunashindwa kuelewa mazingira ya hapa, wengine tumekuja toka asubuhi kufuata fomu hizo, lakini cha kushangaza kuna wengine wamekuja kwa kuchelewa hawajapanga foleni, wanapewa fomu kimjuano wanapitisha tu vikaratasi dirishani,” alisema Jofrey Sichinga.

Aliongeza: “ Tunataka zoezi liendeshwe kihalali kwa sababu ni haki ya kila mtu kupata kiwanja, kwa nini watangulize rushwa kutoa fomu,” alisema.

Aidha, walisema ni bora halmashauri hiyo ingesubiri ijipange vizuri kabla ya kuendesha zoezi hilo ili kuepuka kuwasumbua wananchi kutumia muda mwingi kufuatilia fomu za viwanja wakati viwanja vyenyewe ni vichache.

“Wametangaza kwamba wanatoa fomu za uuzwaji wa viwanja, kumbe viwanja vyenyewe 247 tu na sasa hivi fomu zilizochukuliwa ni zaidi ya 600, huu ni utapeli hizo pesa za fomu tunazolipa wanazipeleka wapi,” alisema Said Dahoma.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Fortunatus Fwema, aliahidi kufuatilia kama kuna ukweli wowote kuhusiana na tuhuma za kuwepo kwa dalili za rushwa katika utoaji wa fomu na kwamba ikithibitika wahusika watachukuliwa hatua kali.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles