Thursday Jun 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

'Utawala Bora nguzo kuu mtangamano wa EAC'

4th June 2012
Print
Comments
Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera

Ikiwa Jumuiya pekee ya kiuchumi katika kanda yenye lengo la kufikia Shirikisho la Kisiasa, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inaona masuala ya utawala bora ikiwa ni pamoja na demokrasia kuwa ni nguzo muhimu katika agenda yake ya mtangamano.

Tamko hili lilitolewa na Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera alipokuwa akifungua mkutano wa Nane wa Jukwaa la  Utawala Bora Afrika lililoandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya EAC, Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Afrika (ECA).

Dk. Sezibera alisema chanzo cha migogoro mingi ya Afrika inatokana na matatizo ya kutokuwepo na utawaala bora na hususan ile inayosukumwa na kasoro katika michakato ya uchaguzi.

“Mambo hayo yanahitaji ushirikiano na mashauriano baina ya watunga sera na wadau wengine ambao hutoa mchango katika masuala ya kukuza demokrasia na matokeo yake,’’ liliripoti Shirika Huru ya Habari ya Afrika Mashariki (EANA).

Dk. Sezibera alisema hakuna budi kuwepo ushiriki wa kutosha wa raia katika masuala ya demokrasia.

Alisema mpango wa EAC wa utawala wa kidemokrasia ni msingi mkubwa katika kufikia lengo la kuweka msingi imara wa Shirikisho la kisiasa, ikiwa ni moja ya nguzo kuu za mtangamano wa EAC.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment