Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Udhamini wa TBL wazua mashaka makubwa Z`bar

29th April 2012
Print
Comments

Klabu zinazoshiriki ligi kuu ya Zanzibar zimeanza kuonyesha mashaka ya matumizi ya fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia (TBL), baada ya kukitaka chama cha soka (ZFA) kuhakikisha zinatumika kwa uwazi na kwa maendeleo ya mchezo pekee.

TBL iliingia mkataba na ZFA wa kudhamini ligi kuu ya Zanzibar kwa sh. milioni 140 kwa mwaka, katikati ya wiki.

Katibu wa timu ya KMKM Sheha Mohamed Ali, alisema udhamini wa TBL utasadia kuinua kiwango cha soka cha Zanzibar iwapo fedha hizo zitatumika kwa uwazi na kusadia kuharakisha maendeleo ya mchezo huo. Alisema KMKM imepokea kwa faraja hatua ya TBL kujitokeza kudhamini ligi kuu ya Zanzibar, lakini uongozi wa ZFA lazima uheshimu masharti ya mkataba pamoja na klabu kushirikishwa kwa karibu katika matumizi.

Katibu wa Mundu, Mcha Mussa Diku alisema jambo la msingi katika udhamini huo kila chombo kijue wajibu wake wakiwemo ZFA, klabu na waamuzi ili kufanikisha malengo ya udhamini huo.

TBl ilisema fedha zitakazotolewa zitakuwa ni kwa ajili ya kugharimia ushiriki wa klabu kwenye ligi kuu hiyo.

Ilisema kampuni hiyo itakuwa ikitoa vifaa, gharama za usafiri, huduma za malazi ugenini na zawadi za washindi wa ligi hiyo. Ligi kuu ya Zanzibar kwa muda mrefu imekosa udhamini kufuatia kujiondoa kwa kampuni moja ya simu baada ya ZFA kupandisha dau la udhamini kutoka sh. milioni 110 hadi sh. milioni 300 mwaka 2008.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles