Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Wabunge CCM wadai serikali ina matumizi mabovu ya fedha

22nd June 2012
Print
Comments
Deo Filikunjombe

Baadhi ya wabunge wa CCM wameiponda serikali kwa matumizi mabaya ya fedha na kumdhalilisha Rais kwa kutembea nchi za nje kuomba fedha wakati nchi ni tajiri kweli.

Wabunge hao, Deo Filikunjombe (Ludewa-CCM) na Maria Hewa (Viti Maalum-CCM)), walisema kwa nyakati tofauti juzi jioni wakati wakichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya serikali iliyowasilishwa bungeni Alhamisi iliyopita na Waziri wa Fedha,  Dk. William Mgimwa.

Akianza Filikunjombe alisema: “Serikali yetu imekuwa na matumizi mabovu ya fedha.”

“Tuwe na nidhamu ya mapato ya fedha zetu…kama hiki kidogo tunashindwa kukitumia ni vipi tukipata kiasi kikubwa,” alihoji.

Alisema wabunge leo wana woga na wasiwasi wakati wakijadili bajeti hii ahadi ambayo serikali ilitoa katika bajeti ya 2011/12 haijatekelezwa.

“Fedha tunapisha, tunapanga, lakini utelezaji wake ni sifuri…kupanga ni kitu kingine na kutekeleza ni kingine pia kwa kuwa serikali yetu imekuwa na matumizi mabovu ya fedha,” alisema.

Alisema sio kwamba serikali haina fedha kwani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakusanya kiwango cha kodi ilichowekewa, lakini serikali inashindwa kuzitumia vizuri.

Alidai kuwa Tanzania inashika nafasi ya tatu baada ya Afghanistan na Iraq kwa kupata misaada mingi ya fedha kutoka nchi licha ya ukweli kwamba Tanzania ina raslimali nyingi ingawa wananchi wake ni maskini.

“Sisi ni matajiri bwana, tuna raslimali kibao,” alisema na kuongeza:Tunamdhalilisha Rais wetu kila siku kwenda nje kuomba fedha…nchi Tajiri, lakini watu wake ni maskini na hii inatokana na kwamba hatuna
matumizi mazuri ya fedha.”

Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msolwa (CCM), alitaka bajeti hiyo ilenge kupunguza umaskini na jambo kubwa la kupunguza umaskini ni kuweka mkazo katika kilimo.






 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment