Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Raia wa Guinea abambwa na dawa za kulevya Dar

20th May 2012
Print
Comments

Raia wa Jamhuri wa Guinea, Marceline Koivogui amekamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, wakati akiwa kwenye harakati za kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine pipi 72 zenye thamani ya Sh. milioni 53 alizokuwa amezificha kwenye sidiria aliyokuwa amevaa.

Kamanda wa Kikosi Maalumu cha Kupambana na dawa za kulevya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Godfrey Nzowa, aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa, mtuhumiwa huyo walimkamata jana majira ya saa 10:00 alfajiri.

Kamanda Nzowa alisema mwanamke huyo walimkamata wakati akiwa kwenye harakati za kusafiri kwa kutumia ndege ya Kenya Airways (KQ) namba 481 ambayo ilikuwa ikielekea Guinee kupitia mjini Nairobi.

Alisema kuwa, katika kitambulisho chake namba 005 kilikuwa kimeandikwa cheo kinachosomeka, Administrateur Civil Matricule huku hati yake ya kusafiria aliyokutwa nayo ilikuwa namba R 0293284.

Alisema kuwa pipi hizo zilikuwa na ukubwa wa gramu 1224 ambapo kwa kawaida kila gramu moja huuzwa Sh. milioni 17. Alisema kwa sasa wanaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo na kwamba upelelezi utakapokamilika watamfikisha mahakamani.

Aidha, Kamanda Nzowa alisema wasafirishwaji wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na hiyo aliyoitumiwa mtuhumiwa huyo.

Alitaja maeneo mengine ambayo watu hao kutumia kuhifadhi dawa hizo kuwa ni kwenye misuli, bandeji na kumeza.

Pia alisema watu hao wamekuwa wakibeba mzigo huo kwa kupokezana kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Alisema taarifa za watu hao wamekuwa wakizipata kwa ushirikiano mkubwa wa ndani na nje ya nchi.

Alisema alitaja baadhi ya nchi ambazo zimekuwa zikisifika kwa kuleta dawa za kulevya ni pamoja na Ghana na Nigeria.

Alisema katika kipindi cha mwaka huu idadi ya wanawake ambao wamekamatwa kwa makosa ya kuingiza dawa za kulevya hapa nchini ni saba ambapo kati yao Watanzania ni watatu.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles