Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Simba yarejea leo kinyonge

15th May 2012
Print
Comments
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage

Simba inatarajiwa kuwasili nchini leo saa tatu asubuhi ikitokea Sudan ilikotolewa katika mashindano Kombe la Shirikisho kwa penalti 9-8 kufuatia kipicho cha magoli 3-0 katika mechi yao ya marudiano dhidi ya Al Ahly Shandy kilichofanya matokeo yao ya jumla kuwa 3-3 kwenye Uwanja wa Shandy juzi Jumapili.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, ambaye ameambatana na timu nchini Sudan, alisema timu inarejea leo na baada ya kufika uongozi utajadili na kutoa ripoti juu ya kilichotokea Sudan.

Simba ambayo ilishinda 3-0 katika mechi yao ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, iliruhusu magoli matatu ndani ya dakika 15 za kwanza za kipindi cha pili, baada ya kucheza vyema katika kipindi cha kwanza kilichomalizika kwa matokeo ya 0-0 na kuleta matumaini kwa klabu hiyo ya Msimbazi.

Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan alisema kuwa Simba ilijiamini mno ndio maana ikashindwa kusonga mbele katika michuano hiyo.

Alisema kwamba akili za wachezaji ziliamini kwamba magoli 3-0 ni mengi jambo ambalo katika soka si sahihi.

Baada ya kuifunga Shandy 3-0 Aprili 29 na kisha kuipa kipigo cha mbwa-mwizi Yanga cha 5-0 huku wakiwa tayari wameshatwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba walikwenda Sudan wakiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele.

Hata hivyo, kukosekana kwa umakini katika safu ya ulinzi, kuliigharimu timu hiyo katika kipigo ambacho kilihitimisha msimu ulioonekana kuwa wa kihistoria kwa wana Msimbazi.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles