Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Uamsho Z`bar yawaponza waasisi

10th June 2012
Print
Comments
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad
Makamu Mwenyekiti wa CCM Amani Abeid Karume

Hatimaye Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara Zanzibar, (JUMIKI) imeanza kuwaponza waasisisi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, (SUK) Makamu Mwenyekiti wa CCM Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad.

Waasisisi hao wametakiwa kuvunja ukimya na kulielezea kinagaubaga suala la Uamsho kama linawakera au wanaliafiki baada ya jumuiya hiyo kuendelea kufanya kampeni za kutaka Zanzibar kujitenga katika mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Taarifa za uhakika toka ndani ya kikoa hicho cha CCM kilichofanyika huko Kinduni Mkoa Kaskazini Unguja juzi zinaeleza jinsi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kaskazini Unguja Haji Juma Haji (Penya) alivyombana Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na kumtaka alifafanue hilo.

Hata hivyo, Vuai alionekana kulikwepa na kulipa mgongo suala hilo na kulikwepa kulitolea majibu suala hilo hata wakati akifanya majumuisho ya mkutano wake wa kukagua uhai wa chama katika mkoa huo.

Penya alisema kuwa ukimya wa viongozi hao wa juu wa kisiasa Zanzibar unatia mashaka hivyo ni vyema wakajitokeza hadharani na kusema ikiwa wanaunga mkono au wanailaani jumuiya hiyo.

Mwenyekiti huyo alisema kwamba Jumuiya hiyo kwa zaidi ya miezi mitano imekuwa ikifanya kampeni za kuvunja muungano na kuchafua hali ya hewa ya kisiasa bila ya kukemewa na viongozi wakuu wa vyama vinavyoounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Alisema kwamba vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na uamsho vina madhara makubwa katika Nyanja ya kiuchumi pamoja na kuyumbisha umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Tanzania.

Inaelezwa kuwa Penya alipoanza kusimama na kuchangia suala la Uamsho alisikika akisema huku akilaumu ukimya wa viongozi hao tokea kuanza kwa harakati za mikutano ya Uamsho na kufanyika kwa maandamano katika mikoa ya Zanzibar.

“Ni kwanini Dk Kaume na Maalim Seif hawataki kulizungumzia suala hili,je wao wanaliafiki au wanalilaani,wajitokeze na kusema ili wananchi wajue mbivu na mbichi”alisemas Mwenyekiti huyo.

Aidha Mwenyekiti huyo wa CCM Kaskazini Unguja pia alihoji ni sababu ipi iliowafanya viongozi wa Uamsho kuamua kukutana na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na kukwepa kukutana na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd hadi sasa wakati ndiyo mtendaji mkuu wa serikali.

“Tulichokiona ni viongozi wa Uamsho akiwemo Farid Hadi na wenzake wakikutana na Maalim Seif, mbona hawajapata shauku ya kukutana na Balozi Seif ambaye ni Mtendaji Mkuu wa kazi za SMZ?”Alihoji huku akishangiliwa na wanaCCM.

Akiizungumzia Jumuiya hiyo Penya alisema yeye kwa upande wake anafikiri kuwa Uamsho imepoteza sifa za kisheria kuwa Jumuiya ya kidini iliosajiliwa kihalali baada ya kuamua kujiingiza katika masuala ya kisiasa na inapaswa kufutwa kwa mujibu wa sheria.

Mwenyekiti huyo wa CCM alimtaka Waziri wa Katiba na Sheria Abobakary Khamis Bakary kujiuzulu wadhifa wake kwa kushindwa kuishauri vizuri serikali kuhusu sheria na katiba na kusababisdha vurugu na makanisa kuchomwa moto Zanzibar.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment