Monday May 2, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Wafadhili wadaiwa kuwapa wakati mgumu walimu

24th May 2012
Print
Comments
Walimu mablimbali wa shule za msingi na sekondari

Walimu wa shule za msingi na sekondari zilizopo wilayani Karatu, mkoa wa Arusha zinazofadhiliwa na wafadhili kutoka nje wanakabiliwa na utendaji mgumu wa kazi kutokana na baadhi ya wafadhili kuwaingilia kimaamuzi katika uendeshaji wa shule hizo hali ambayo imesababisha kuporomoka kwa kiwango cha elimu wilayani humo.

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Karatu, Peter Simwanza, amebainisha hayo wakati akizungumza na NIPASHE jiji Dar es Salaam jana, kuhusu changamoto zinazoikabili sekta ya elimu wilayani humo.

Simwanza alitoa mfano kuwa baadhi ya wafadhili wanakataa masomo fulani yasifundishwe katika shule hizo wanazozifadhili kitu ambacho ni kinyume na sheria za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Alisema walimu wanaposhikilia msimamo wa kukataa matakwa ya wafadhili hao wanakwenda kushinikiza kwa viongozi wa Idara ya Elimu ili walimu hao wahamishwe katika shule hizo kwa madai kwamba wanawakwaza kutokana na kutokubaliana na matakwa yao.

Katibu huyo wa CWT alisema kutokana na mashinikizo hayo ya wafadhili, baadhi ya walimu ambao wamehamishwa bila utaratibu, kumekuwa na mlundikano wa madai ya walimu wanaodai stahiki zao baada ya kuhamishwa kwa shinikizo la wafadhili hao.

Simwanza alisema katika kukabiliana na matizo hayo, Chama cha Walimu Tanzania kimekuwa kikichukua hatua kadhaa ikiwemo kuwaelimisha walimu kutambua haki zao na kuzidai kwa nguvu zote.

Katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo mwaka 2007, 2009 na 2010 wilaya ya Karatu ambayo ni miongoni mwa wilaya sita za mkoa wa Arusha ilishika nafasi ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles