Wednesday Jun 19, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mwingine ajitosa kupambana na Sophia Simba

4th August 2012
Print
Comments
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba

Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mayrose Majinge, amejitosa kugombea uenyekiti wa Umoja wa Wanawake Nchini wa chama hicho (UWT).

Kuchukua fomu kwa kada huyo, kunafanya jumla ya wanachama wa chama hicho wanaowania nafasi hiyo kufikia watatu katika ofisi za makao makuu ya chama hicho mkoani Dodoma.

Wengine waliochukua fomu mkoani hapa ni Mwenyekiti wa sasa wa UWT, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela.

Akikabidhiwa fomu hizo jana, Mayrose alisema ameshawishika kutokana na kuwa na sifa za kimaadili, elimu ya kutosha rasmi na isiyo rasmi na maarifa.

“Ni haki yangu kimsingi ya kikatiba kugombea nafasi hii, ninaruhusiwa kugombea kwa mujibu wa Katiba ya nchi na a UWT,” alisema Mayrose aliyekuwa ameongozana mumewe Joseph Kusaga.

Mayrose alisema amewahi kushika nyazifa mbalimbali ndani ya chama  ikiwemo kuwa Katibu wa chama hicho katika Shule ya Sekondari ya Mwanza, mjumbe wqa Baraza Kuu la UVCC na Katibu wa UVCCM wilaya ya Ilala.

Pia aliwahi kushiriki katika michakato mbalimbali ikiwa ni pamoja na kugombea ubunge wa Afrika Mashariki, ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Alisema iwapo atapata ridhaa ya wanachama kuongoza jumuiya hiyo, atashughulikia changamoto kubwa ya uchumi inayowakabili wananchi nchini.

Alipoulizwa kuhusu iwapo anahofia kupambana na makada wakubwa waliochukua fomu, Mayrose alisema mtu anayeogopa hafai kuwania nafasi yoyote ya uongozi.

“Siwezi kuogopa, huwezi kuitwa kiongozi kama unaogopa, mimi ni kijana na kijana huwa unakuwa mwepesi zaidi na sioni kwamba kuwania nafasi hii ni suala la uzoefu bali ni sifa na uwezo,” alisema.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment