Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Chadema yavuna TLP

24th April 2012
Print
Comments

Katibu wa Chama Cha Tanzania Lebour (TLP) Jimbo la Songea mkoani Ruvuma, Joseph Mkondora, amejitangaza kujivua uwanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkondora alisema amechukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa Chadema ndicho chama pekee cha upinzani kinachoonyesha dira ya maendeleo kwa Watanzania.

Mkondora alisema kuwa ameamua kujivua uananchama wa TLP kwa sababu Mwenyekiti wa TLP Taifa, Augustine Mrema, tangu achaguliwe kuwa mbunge ameshindwa kufuatilia uhai wa chama, hali iliyosababisha kudorora kwa shughuli katika Jimbo la Songea Mjini.

Mkondora slisema  kuw TLP katika jimbo hilo kila uchao kinapoteza wanachama na kwamba  taarifa zimekuwa zikipelekwa makao makuu, lakini viongozi wamekaa kimya. “Ndugu waandishi hali ya TLP awali ilikuwa na wanachama zaidi ya elfu saba, lakini hivi sasa chama hicho kimebakiwa na wanachama kumi na moja tu,” alisema Mkondora.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles