Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

LAAC yacharukia Halmashauri ya Tarime

8th June 2012
Print
Comments
Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Idd Azzan

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabau za Serikali za Mitaa (LAAC) imeendelea kucharuka baada ya kuutimua uongozi wa Halmashauiri ya Wilaya ya Tarime kwa kushindwa kuandaa hesabu vizuri pamoja na kuagiza asilimia 15 ya mshahara wa mkurugenzi wake ukatwe.

Agizo hilo lilitolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Idd Azzan, alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema kamati yake haijaridhishwa na mpangilio wa vitabu vya mahesabu vya wilaya hiyo kwa sababu kuna vitu havieleweki namna vilivyofanyika.

Wengine watakaokumbwa na adhabu hiyo ni Mweka Mazina wa Halmashauri hiyo, Elias Ameda na Mkaguzi wa Ndani, Joas Maganga.

Azzan alisema katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Bukenye-Ekerege yenye urefu wa kilometa 46, iligharimu Sh. milioni 239, lakini hakuna mchanganuo wa matumizi pamoja na sehemu aliyosaini mkandarasi wa barabara hiyo.

Alisema barabara hiyo ilipewa wakandarasi wawili kuijenga, lakini hapakuwapo na sehemu waliyosaini wakandarasi hao.

Kamati hiyo ilishtushwa na matumizi ya Sh. milioni 50 zilizotumika katika ukarabati wa vyoo, majiko na ujenzi wa matundu ya vyoo viwili katika Shule ya Sekondari Tarime.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment