Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Papic aenda Mwanza kwa nguvu

15th April 2012
Print
Comments
Kocha mkuu wa Yanga Kostadian Papic

Kocha mkuu wa Yanga Kostadian Papic anaondoka leo jijini kwa ndege kwenda Mwanza kuungana na timu hiyo inayocheza na Toto African katika mchezo wa ligi kuu ya Bara, kinyume na maelezo ya uongozi kuwa mwalimu huyo ni mgonjwa na hatosafiri.

Yanga na Papic ambaye amekaririwa akilalamika kutolipwa mshahara kwa miezi mitatu kabla ya madai hayo kukanushwa, wapo katika mgogoro wa chini kwa chini wakati pande hizo zikiwa zimebakiza siku tisa za mkataba baina yao.

Aidha, Mserbia Papic alisema jana kuwa anajiandaa kurudi nyumbani baada ya kumalizika kwa mkataba huo.

Na kusafiri kwa kocha huyo wakati uongozi ukitaka abaki Dar es Salaam ni ishara nyingine kwamba huenda kilichobaki sasa ni kuonyeshana mabavu.

Mapema jana, Katibu wa Yanga Celestine Mwesigwe alisema kocha huyo ameshindwa kwenda Mwanza kuungana na timu kwa ajili ya mchezo wa leo wa ligi kuu dhidi ya Toto African kwa kuwa hajapata nafuu kutokana na kuumwa mafua pamoja na maumivu ya tumbo.

"Kocha hawezi kwenda Mwanza kwa sababu hajapona... tulifikiria labda mpaka kufika jana (Ijumaa) angekuwa amepona lakini imeshindikana," alisema Mwesigwe. "Timu itakuwa chini ya (kocha msaidizi Fred Felix) Minziro."

Hata hivyo alipozungumza kwa simu na Nipashe jumapili baadaye, Papic alisema ataondoka leo asubuhi kwa ndege kuungana na timu hiyo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

"Ilikuwa niondoke leo (jana) lakini safari imeairishwa na sasa nitaondoka kesho asubuhi kwenda Mwanza kuungana na timu," alisema Papic.

Alisema kuwa kwa sasa anajisikia kupona baada ya kupata matibabu na kusisitiza leo asubuhi "nakwenda Mwanza kuungana na timu."

Papic alisema mkataba wake na Yanga unamalizika ndani ya siku 10 kuanzia jana na kwamba siku hiyo ya mwisho "nitakuwa tayari kuwaambia viongozi wa Yanga kuwa sihitaji tena kazi. "Kwa kweli sipo tayari kuendelea na kazi na Yanga... baada ya kumalizika mkataba nitarudi nyumbani (Serbia) na tayari nimeanza kujiandaa kuondoka."

Mkataba wa koch a huyo unamalizika Aprili 24 lakini Yanga ambayo ni ya tatu kwenye ligi inayotetea ubingwa ikiwa na pointi 43, saba nyuma ya viongozi na ikiwa imebaki za michezo mitano, itapambana na Simba Mei 5.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles