Thursday May 5, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mawaziri wapya safi, tuangalie kwanini mivutano inazidi

6th May 2012
Print
Comments
Maoni ya Mhariri

Rais Jakaya Kikwete amekamilisha kazi ya kuteua baraza jipya la mawaziri, ukiwemo uteuzi wa wanataaluma waliteuliwa ubunge na kupata uwaziri, halafu manaibu waziri walipewa majukumu mapya.

Kila mmoja atakuwa na hisia zake kuhusu uteuzi, na kwa kawaida kwa mambo kama hayo inakuwa ‘hakuna kulazimishana’ maoni.

Hata wale ambao wametemwa, ukiangalia kwa karibu ni matatizo ya mfumo pamoja na uongozi wa juu kuchagua nini kifanye, na nini kiache. Maamuzi yake yanaweza kukiuka matarajio.

Isitoshe kuna matazamio ya kinyemela katika ngazi tofauti za utawala, yanayotokana na matabaka tofauti kutoridhika na wanachopata. Kutazamia kuwa kila kundi la jamii lazima liridhike na lilichopewa katika Bajeti ni kutokuelewa utawala, kwani mpaka waingie barabarani mara nyingine mambo yameshahabiribika maeneo fulani.

Tuchukulie kwa mfano wakati wa Ujamaa. Hapakuwahi kuwa na maandamano ya wafanyakazi wa sekta hii au ile lakini takriban makampuni 400 ya taifa (mengine ‘mashirika’) yalididimia, ikabidi tu yafungwe.

Malumbano yanayotokea sasa hivi bungeni kuhusu utendaji serikalini una vianzio vya aina takriban tatu, ya kwanza ikiwa ni kupungua kwa mamlaka ya mkuu wa nchi na vitisho vya dola, kwa mfano kukamatwa na polisi wa upelelezi kueleza fedha ilivyopotea. Hivi sasa mtu akikamatwa hivyo anahojiwa kiungwana anafunguliwa mashtaka – zamani ilikuwa tofauti kidogo, kwa upande wa haki za binadamu. Hofu hiyo pia huchangiwa na ujio wa vyama vingi, ambao huinua ulaghai wa kukwepa anachojua waziri, umbamize.

Kianzio cha mwisho kinaonekana kikubwa zaidi, nacho ni jinsi ya kutawala mikataba ya makampuni tofauti na kufanya malipo, ambacho kwa upande fulani kinachangiwa na hali kuwa ni eneo pana linalowezesha ugeuzaji wa mwelekeo wa mabilioni ya pesa.

Watu wakisikia hilo limefanyika wanadhani ni wizi, lakini waziri atakaaje kwenye kiti afikie kutia hasara serikali shilingi bilioni 300 bado hakuna taasisi za nchi - fedha, usalama, benki kuu, watendaji waandamizi wizarani – hadi ihojiwe na kuchunguzwa bungeni? Na ikiwa wapinzani na wabunge wa CCM wanajua hilo lakini hawalisemi, si kufaidika kura?

Kuna kianzio kingine kinacholeta hili la maslahi yanayotokana na ‘kashfa’ kuwa kama petroli imemwagika halafu mtu amewasha kiberiti, yaani wingi wa mikataba unazuia hata waziri asijue kila chembe ila mistari muhimu zaidi.

Halafu mashindano ya kimaslahi kati ya watawala yanazidi. Kwa mfano mwaka jana mwishoni wabunge walikuwa wamepania kuongezewa posho kutoka Sh.70,000 kwa siku ya mkutano hadi laki mbili, maamuzi ambayo kimsingi yalikuwa na ridhaa yote ya Bunge.

Rais Kikwete akiwa amejua hali ya hisia ilivyo kuhusu suala hilo akaliweka pembeni akitaka busara. Wakati bado mivutano inaendelea huko, madaktari wakaanza migomo, wabunge wakajua ‘uji umemwagika.’ Lakini wakaelekeza hasira zao serikalini; mawaziri ‘wanakula’ huku wao wamenuna!

Hivyo ukisikia waziri huyu au yule ambaye anajua fika anatazamiwa na uongozi wa juu Baraza la Mawaziri eti hakutambua wajibu wake ila ni wabunge ‘wakali’ wa CCM na wale wa upinzani, tena mara nyingine kwa majina yale yale wakipokezana, ni vyema kutilia shaka kinachozungumzwa.

Kwa msingi huo, ndio maana tunasema kuwa anayejua taratibu za maamuzi na ufuatiliaji serikalini anafahamu kuwa kuafikiwa malipo ya aina moja au nyingine ni shughuli pevu, na hundi hiyo ianze au ikamilike kulipwa iko ‘mikono’ mingi inayotakiwa ‘kuanguka.’

Kwa hiyo, udhania kuwa watu kama hawa wanatia saini mambo yaliyokubaliwa katika mgahawa wa hoteli maarufu ni kutokuielewa serikali, kuwa makundi kadhaa yalihitaji alichofanya waziri.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles