Wednesday May 22, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Polisi kuzungumzia wabunge wa Chadema waliojeruhiwa

25th April 2012
Print
Comments
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk.Willibroad Slaa

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, leo linatarajia kutoa taarifa rasmi kuhusu hatua zilizokwishachukuliwa dhidi ya watuhumiwa wanaodaiwa kuhusika katika tukio la kuwacharanga mapanga Wabunge wa Chadema, Highness Kiwia wa Ilemela na Salvatory Machemli wa Ukerewe.

Hatua hiyo ya Polisi inakuja wakati ambapo Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk.Willibroad Slaa, ametoa siku saba kwa jeshi hilo kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wote wanaotajwa kuhusika katika tukio hilo.

Akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jumapili iliyopita jijini hapa, Dk. Slaa alionya kwamba iwapo Jeshi la Polisi litashindwa kuwachukulia hatua watuhumiwa hao, basi atahamasisha wananchi kuteka kituo cha polisi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Phillip Kalangi, alisema kuwa leo ndiyo siku ambayo anaweza kutoaa taarifa kamili kuhusu hatua zilizokwishachukuliwa dhidi ya watu wanaodaiwa kuwacharanga mapanga wabunge hao.

“Tutatoa taarifa kamili kesho (leo), kwani bado kuna masuala tunafuatilia na hayajakamilika, lakini hadi kesho tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kusema chochote,” alisema.

Tangu wabunge hao walipocharangwa mapanga mwanzoni mwa mwezi huu, kumekuwepo na lawama kutoka kwa viongozi wa Chadema dhidi ya Jeshi la Polisi kushindwa kuwachukulia hatua watu waliotajwa kuhusika.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment