


Kampuni ya kimataifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Mahesabu ya KPMG, ya Uingereza imeteuliwa kufanya tathmini ya mali za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) ikiwa ni makubaliano ya kumaliza mgogoro muda mrefu wa ubinafusishaji wa shirika hilo.
Serikali serilikubaliana na mwekezaji kampuni ya Simon Group kuthamini maliza za shirika hilo ili kwenda sawa na soko.
Meneja Mawasiliano wa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya umma (CHC), Joseph Mapunda, amethibitisha kuwepo kwa makubaliano hayo kati ya serikali na Simon Group, na kwamba CHC imeiteua kampuni ya KPMG yenye tawi lake nchini.
“Kwa sasa siwezi kukueleza chochote kuhusu utamini kwani bado haujakamilika na sisi CHC na tukikabidhiwa ripoti ya uthamini toka KPMG tutawaeleza,” alisema Mapunda.
Mkurugenzi wa KPMG Keton Shar alipoulizwa kuhusu zoezi hili alisema hawezi kusema lolote kwani kazi haijamalizika.
“Lakini wewe unajua kuwa sisi hatuwezi kuzungumza kazi za wateja wetu bila wao kuturuhusu ili ni kweli kazi tunaifanya ikimalizika tutapeleka ripoti kwa mteja wetu nae atawapa majibu,” alisema mkurugenzi huyo.