Tuesday May 3, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

CAG sasa kuanika uozo wa halmashauri ALAT

25th April 2012
Print
Comments
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh

Uozo wa halmashauri unaohusisha ufisadi wa mabilioni ya fedha, utaanikwa tena katika Mkutano Mkuu wa 28 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) utakaofunguliwa na Rais Jakaya Kikwete na kuhudhuriwa na mawaziri 11, akiwamo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika.

Uozo huo wa halmashauri, utaanikwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, katika mkutano unaotarajiwa kuhudhuriwa na washiriki 500.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa ALAT, Dk. Didas Masaburi, mkutano huo utafanyika Mei 3-5, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, ambapo maandalizi yake yanatarajiwa kugharimu Sh. milioni 500.

Dk. Masaburi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Utouh ni miongoni mwa viongozi mashuhuri walioalikwa na jumuiya hiyo kushiriki mkutano huo.

Taarifa hiyo iliwasilishwa na CAG bungeni hivi karibuni na kuanika ufisadi wa kutisha wa fedha za serikali.
Taarifa hiyo CAG pamoja na mambo mengine, ilionyesha kuwa deni la taifa limeongezeka kutoka Sh trilioni 10.5 mwaka juzi na kufikia Sh trilioni 14.4 mwaka jana.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali ilitumia Sh. bilioni 544 bila kuidhinishwa na Bunge, Sh. bilioni moja zimelipwa mishahara kwa watumishi hewa na Sh. bilioni 3 zimetumika katika Balozi za Tanzania nje ya nchi ambazo ziko nje ya bajeti na misamaha ya kodi ya Sh trilioni 1.02.

Wengine watakaoshiriki ni mameya wa halmashauri zote 133 za majiji, manispaa, miji na wilaya, wakurugenzi wa halmashauri (ma-DED) zote nchini, wabunge 21 (mmoja kutoka katika kila mkoa).

Mawaziri walioalikwa ni Mkulo Ngeleja; Mkuchika; Gaudentia Kabaka (Kazi na Ajira) na Dk. Emmanuel Nchimbi (Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo). Wengine ni Profesa Anna Tibaijuka (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi); Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii); Dk. Chami; Shamsi Vuai Nahodha (Mambo ya Ndani ya Nchi); Profesa Jumanne Maghembe (Kilimo, Chakula na Ushirika) na Dk. Mathayo David (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi).

“Tunachotaka ni mwelekeo na mikakati ya serikali ili kuona namna serikali za mitaa zitakavyojipangia malengo yake na kutekeleza,” alisema.

Alisema jukwaa hilo litajadili mada mbalimbali zinazohusu ubia; ambazo ni pamoja na maana halisi ya ubia, je, ni ubinafsishaji?; Njia mbalimbali za kufanya ubia; msingi wa kisheria wa ubia; uzoefu wa hali halisi ya ubia kimataifa; dhati/dhamira hasa ya ubia; na faida zinazoweza kupatikana kutokana na ubia.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles