Thursday May 5, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Tantrade, Dubai zaingia mkataba

17th May 2012
Print
Comments
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu

Mamalaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), imesaini hati ya makubaliano na Wakala wa uhamasishaji uuzaji wa bidhaa za nje wa Nchini Dubai, kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya pande zote mbili pamoja na kuhamasisha uwekezaji.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu alizitaka nchi za Uarabuni kuwekeza  nchini kwa kuwa  itasaidia kuongeza uzalishaji na hivyo kuuza zaidi bidhaa kuliko kununua.

"Nchi za Uarabuni zina hela, zikiwekeza kwetu zitatusaidia tuongeze uzalishaji na tuwe wauzaji zaidi kwa hiyo makubaliano haya yatatusaidia kuwa na biashara yenye faida," alisema Nagu.

Awali akizungumza katika hafla hiyo iliyowakutanisha wafanyabiashara mbalimbali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dubai Exports, Mhandisi Saed Al Awadi, alisema mpango huo wa biashara na Tanzania ni moja ya juhudi zao katika kusaidia wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa zao kwenda nje ya nchi ili kukuza soko la Afrika ambalo linakua kwa kasi.

"Tunaamini kuwa bara la Afrika ni soko muhimu kwa bidhaa zinazotoka Dubai, uhusiano wa kidugu na wa muda mrefu kati yetu utawapa wafanyabiashara wetu msingi imara," alisema Awadi.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, alisema serikali inapaswa kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya wawekezaji ikiwa ni pamoja na kuwasisitiza wafanyabiashara wa hapa nchini kufanya biashara nzuri ili kukuza uchumi wa nchi.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles