Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Rais Kikwete aweka historia mkutano wa G-8

21st May 2012
Print
Comments
Rais Jakaya Kikwete wa nne kulia akiwa na miongoni mwa Marais wanaohudhuria mkutano wa nchi nane tayari duniani wanajulikana kama G-8, ulioitishwa na Rais wa Marekani Barak Obama wa kuzungumzia hali ya chakula duniani.

Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi wengine wa nchi za Afrika wameweka historia baada ya kuhudhuria kwa mara ya kwanza mkutano wa Nchi nane tajiri duniani (G-8), ambao ulifanyika Camp David katika jimbo la Maryland nchini Marekani.

Viongozi wengine wa Afrika waliopata fursa ya kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, Rais wa Ghana, John Atta Millls na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Benin Yayi Boni.

Mkutano huo ulifanyika juzi nchini Marekani ambapo imeelezwa kwamba tukio hilo limewekwa katika vitabu vya kumbukumbu.

Mkutano huo uliandaliwa na Rais wa Marekani, Barack Obama na alitangaza kuzisaidia nchi za Afrika Dola za Marekani bilioni tatu kwa ajili ya kuwekeza katika kilimo.

Licha ya viongozi wa G-8 pamoja na  viongozi wanne wa Afrika pia mkutano huo ulihudhuriwa na watu sita maarufu miongoni mwa Wamarekani ambapo waliazimia kuunda umoja kwa ajili ya kuangalia suala la chakula na lishe.

Rais Obama alisema anaamini kwamba ni mara ya kwanza sekta binafsi kushirikishwa ambapo mtendaji mkuu wa PepsiCo, Indra Nooyi naye alihudhuria mkutano huo muhimu ambao uliangalia masuala ya chakula.

Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Stephen Harper, Waziri Mkuu wa Canada, Rais Ufaransa, François Hollande na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.

Wengine ni Mawaziri wakuu wa nchi za Italia, Mario Monti, Japan , Yoshihiko Noda, Urusi,   Dmitry Medvedev pamoja na  Uingereza, David Cameron   

"Hii ni mara ya kwanza mkutano wa G-8 kuhusisha viongozi wengi pia kuwa viongozi wa NGOs na viongozi wa wafanyabishara," alisema Obama.

Umoja mpya ulioundwa utasaidia kuanzisha juhudi za usalama wa chakula ambazo mwaka 2009 viongozi wa G-8 walitoa dola za Marekani bilioni 22.

Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani waliohudhuria mkutano huo kutoka sekta binafsi ni pamoja Nooyi ambaye ni mwenyekiti na mtendaji mkuu wa PepsiCo na  Michael Mack, ambaye ni mtendaji mkuu wa  Syngenta International AG.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles