Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Wasiogoma watishiwa

1st August 2012
Print
Comments
Baadhi ya Walimu

Baadhi ya walimu wilayani Bunda, mkoani Mara, wanaoshiriki kwenye mgomo ulioanza juzi, wamesema wenzao watakao kataa kugoma, watawashambulia kwa mawe kwa sababu watakuwa wanawasaliti.

Baadhi ya walimu walisema iwapo walimu wenzao watathubutu kuingia madarasani wanafunzi, watawashambulia kwa kuwapiga mawe kwani watakuwa wasaliti.

Hadi juzi na jana baadhi ya shule wilayani wanafunzi walikuwa madarasani bila ya kuwepo walimu huku wanafunzi wengine wakitangatanga.

Baadhi ya walimu waliofika kwenye vituo vyao vya kazi asubuhi na baadaye kuwaacha wanafunzi madarasani.

Mwenyekiti wa CWT, mkoani Mara, Livingstone Gamba, alisema kuwa tayari walimu wote mkoani hapa wameshiriki kwenye mgomo huo usiokuwa na kikomo.






 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment