Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Ngorongoro wapaa Sudan, waahidi ushindi

3rd May 2012
Print
Comments
Kocha Mdenmark Kim Poulsen

Timu ya soka ya vijana wa umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) iliondoka nchini jana mchana na kuelekea Sudan huku kocha Mdenmark Kim Poulsen na wachezaji wake wakiahidi kwenda kutafuta matokeo mazuri ili waweze kusonga mbele katika mashindano hayo ya vijana ya Afrika.

Ngorongoro itakutana na wenyeji wao keshokutwa Jumamosi kuanzia saa 2:00 usiku kwenye Uwanja wa Khartoum.

Akizungumza jana muda mfupi kabla hawajaoondoka nchini, Kim alisema kuwa wanaenda kupambana kwa lengo kushinda katika mechi hiyo ya marudiano kama walivyofanya katika mechi yao ya awali.

Katika mechi ya kwanza iliyofanyika hapa nyumbani Ngorongoro Heroes iliwafunga Sudan 3-1 na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kucheza hatua ya pili.

Kim alisema kuwa wanaenda kumalizia kazi waliyoianza vyema hapa nyumbani na kushinda kutawafanya waweze kusonga mbele huku wakijiamini zaidi.

"Tumejiandaa vizuri na mchezo wetu, tuko tayari na tunataka kuendeleza wimbi la ushindi, hatutabweteka, tutafanya mashambulizi ya mara kwa mara ili kusaka magoli zaidi," alisema kocha huyo.

Naye nahodha wa timu hiyo, Omega Seme, alisema kuwa timu imefanya mazoezi kwa muda mrefu na wakiwa Sudan wanaahidi kupambana ili kuweza kushinda.

"Kama wachezaji tunawaahidi hatutawaangusha, lengo letu ni kushinda na kusonga mbele," Seme aliongeza.

Timu hizo zinakutana katika mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika baadaye mwaka huu nchini Algeria.

Yosso hao wa Tanzania wakiitoa Sudan watakutana na timu ya vijana ya Nigeria Julai 28 jijini Dar es Salaam na mechi ya marudiano itafanyika Nigeria kati ya Agosti 10 na 12 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah, ambaye amerejea kazini baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa, ndiye aliyekabidhi bendera kwa vijana hao na kuongeza kuwa taarifa walizonazo Khartoum hakuna machafuko na hata Rais wa TFF, Leodegar Tenga yuko Sudan Kusini akisimamia uchaguzi wa chama kipya cha soka cha nchi hiyo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles