Thursday May 5, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Wakewenza kutibiwa NHIF Z'bar kwazua utata

28th April 2012
Print
Comments
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Tanzania, (NHIF)

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Tanzania,  (NHIF) umesema kwamba suala la wake wenza Zanzibar kuingizwa katika utaratibu wa kunufaika na mfuko huo halihitaji haraka kutokana na unyeti wake.

Tamko hilo limetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Emmanuel Humba, alipokuwa akizungumza na wanachama wa NHIF kanda ya Zanzibar mjini Zanzibar jana.

Alisema kwa mujibu wa sheria ya mfuko huo, kila mwanachama anatakiwa kunufaika na matibabu wakiwemo wategemezi wake wanne, (watoto) mke mmoja na yeye mwenyewe.

Hata hivyo, alisema kwamba wanachama wenye wake wenza wanayo nafasi ya kunufaika na matibabu kama mke mmoja au wawili hatawaingiza katika kundi la wategemezi wake.

Alisema kwamba uongozi wa mfuko huo upo makini katika kujadili mambo yenye mtazamo wa  dini na ndiyo maana wamekuwa wakiwashirikisha viongozi wa dini katika kujadili mambo kama hayo.

Awali wanachama wa mfuko huo walitaka kujua uongozi wa NHIF una mpango gani wa kuhakikisha wakewenza wote wananufaika na matibabu badala ya mke mmoja.

Hata hivyo, Humba alisema kwamba wazo hilo, limepokelewa na uongozi wa NHIF utalifanyia kazi na kuwataka wanachama wa mfuko huo kuwa na subira wakati bodi ya mfuko ikifanyia kazi tatizo hilo.

Kuhusu SMZ kuwa na mpango wa kuanzisha Mfuko kama huo, Mkurugenzi huyo alisema kwamba hatua hiyo haina athari yoyote kwa NHIF kwa vile mfuko huo haumo katika orodha ya mambo ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Alisema kwamba watumishi ambao wamekuwa wakinufaika na mfuko huo ni watumishi wa Taasisi za muungano wakiwemo askari wa Vikosi vya ulinzi na usalama.

Upande wake Meneja wa NHIF kanda ya Zanzibar, Peter Daniel alisema kwamba kumeibuka vitendo vya utapeli kwa baadhi ya vituo vilivyosajiliwa kuandaa madai ya kugushi kitendo ambacho kinyume na sheria.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles