Sunday May 26, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Azam yapania kuifunga Tusker

21st July 2012
Print
Comments
Kocha Azam FC, Stewart Hall

Kocha Azam FC, Stewart Hall, amesema kuwa timu yake imepania kuwafunga mabingwa wa Kenya, Tusker wakati ikitafuta kufuzu kucheza robo-fainali ya michuano ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati ambapo upo uwezekano wa kukutana na Simba.

Endapo Azam itashinda na kuchukua nafasi ya kwanza katika Kundi B, itakutana na mshindi wa pili wa Kundi A inayowaniwa na timu mbili ngumu -- Simba na APR ya Rwanda zitakazocheza pia leo.

Simba na Azam zimeshakutana mara mbili mwezi huu na kutoka sare katika michezo yote hiyo ya maandalizi ya msimu mpya, ingawa kwa rekodi Simba ilishinda kwa matuta na kutwaa Kombe la Urafiki siku 10 zilizopita.

Baada ya kikosi hicho cha Azam kutoka sare ya bao 1-1 na Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa kwanza, na Wakenya hao kutoka suluhu katika mchezo dhidi ya Wazanzibari, Azam inataka kuepuka matokeo ya tatu mfululizo ya kufanana katika Kundi B.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kati ya Tusker na Mafunzo, Hall alisema kuwa hana shaka na mchezo wao dhidi ya Tusker kwa kuwa amewaona dhidi ya Mafunzo na kusema kuwa amewaandalia mbinu za kuhakikisha wanaibuka na ushindi utakaowapeleka kwenye robo fainali.

"Nimewaona Tusker, nimeona ubora wao na mapungufu yao... najua tuna kazi lakini sina shaka na timu yangu. Tutahakikisha tunaibuka na ushindi ili tusonge mbele," alisema Hall.

Aidha, alisema kuwa baada ya michezo ya makundi hatua robo fainali itakuwa ngumu kwa kuwa timu zote zitakazotinga zitakuwa zimejiimarisha zaidi.

Hall alisema yupo tayari kucheza na timu yoyote watakayokutana nayo baada ya kuvuka hatua ya makundi, hata hivyo.

Hall alisema leo hawatafanya makosa waliyoyafanya kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mafunzo.




 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment