Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Taifa Stars wajionea tofauti kwa Poulsen

20th May 2012
Print
Comments
Kim Poulsen

Wachezaji wa timu ya soka ya taifa 'Taifa Stars' walisema wameona tofauti kati ya kocha wa sasa, Kim Poulsen na mtangulizi wake Jan Poulsen.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wachezaji hao walisema kocha wa sasa Kim yupo karibu na wachezaji.

Mmoja wa wachezaji wa muda mrefu wa Stars ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema kwa kipindi kifupi ambacho kocha huyo amefundisha, Kim amekuwa karibu na wachezaji.

"Mabadiliko yapo... Kim ni kama rafiki. Yupo karibu na wachezaji," alisema na alipotakiwa kueleza tofauti ya kifundi alijibu "ni mapema lakini... tusubiri tuone."

Mchezaji huyo alisema wanategemea makubwa kutoka kwa kocha huyo lakini akasisitiza wachezaji kwenye timu hiyo ya taifa wanapaswa kujituma ili kuipa mafanikio.

"Hata kama kocha atakuwa mzuri vipi kama sisi wachezaji hatutojituma uzuri wa kocha hautoonekana," alisema.

Mchezaji mwengine alisema kwake ni mapema kujua utofauti wa kocha wa sasa wa timu hiyo na kocha aliyepita lakini akasema kuwa kwa muda mfupi kocha huyo amekuwa karibu na wachezaji huku akisisitiza nidhamu na kujituma.

Kim ameichukua timu hiyo ya taifa baada ya shirikisho la soka (TFF) kutomuongeza mkataba Jan Poulsen.

Kim na kikosi chake yupo kambini kujiandaa kwa mchezo wa michuano ya awali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast utakaofanyika Juni 2 jijini Abidjan.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles