Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Ajali ya lori, daladala yaua watatu, kujeruhi wanane Dar

22nd June 2012
Print
Comments
Wapita njia wakiangalia basi la daladala lililogongwa na lori eneo la Tegeta Kibaoni, jijini Dar es Salaam jana. Watu wawili walikufa kwa kugongwa na lori hilo na abiria wanane wa basi

Watu watatu wamefariki dunia na wengine nane kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha lori na daladala katika eneo la njia panda ya Wazo na Tegeta, jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela, alisema ajali hiyo ilitokea jana asubuhi baada ya lori kuligonga daladala lililokuwa limeegeshwa ambapo pia sehemu baa ya KMKM pamoja na duka vilibomolewa.

Aliwataja waliofariki kuwa ni Halima Msoro (35- 40) aliyekuwa mamalishe katika baa hiyo na mwanaume mpita njia, ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

Habari zilizopatikana wakati tukienda mitamboni, zinaeleza kuwa mtu mwingine wa tatu alifariki dunia njiani wakati akipelekwa hospitali. Hata hivyo, zilikanushwa na Kamanda Kenyela.

Kenyela alisema chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa breki za lori aina ya tipper Scania, lililokuwa likitokea katika Kiwanda cha Saruji cha Wazo, na hivyo kuvamia daladala hilo hilo aina ya Isuzu Journey linalofanya safari Kariakoo- Tegeta, lililokuwa linapakia abiria sehemu, ambayo hairuhusiwi.

Kenyela alisema majeruhi, walipelekwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles