Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Twiga Stars kambini leo

20th April 2012
Print
Comments
Timu ya soka ya Tanzania ya wanawake (Twiga Stars)

Timu ya soka ya Tanzania ya wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuingia kambini leo ikiwa chini ya kocha wake, Charles Boniface Mkwasa kujiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Zimbabwe inayofanyika Aprili 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Twiga Stars kabla ya mechi ya mashindano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia itakayochezwa Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa na baadaye timu hizo kurudiana hapa jijini Dar es Salaam.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema jana kuwa baada ya wachezaji kuripoti kambini jioni, kesho wataenda kufanyiwa vipimo vya afyana mazoezi yataanza Jumapili.
Kambi ya timu hiyo itakuwa kwenye hosteli za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Ruvu mkoani Pwani.

Aliwataja wachezaji walioitwa ni Amina Ally kutoka Sekondari ya Lord Baden, Asha Rashid, Aziza Mwadini (New Generation, Zanzibar), Etoe Mlenzi (JKT Mbweni), Evelyne Sekikuto (Mburahati Queens), Fadhila Hamad (Uzuri Queens), Fatuma Bashiri (Simba Queens), Fatuma Khatib (Mburahati Queens), Fatuma Mustafa (Sayari), Fatuma Omari (Sayari), Hanifa Idd (Uzuri Queens) na Maimuna Said wa JKT Mbweni.

Wachezaji wengine ni Mariam Aziz (Tanzanite), Mwajuma Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens), Mwapewa Mtumwa (Sayari), Rehema Abdul (Lord Baden), Rukia Khamis (Sayari), Semeni Abeid (Tanzanite), Siajabu Hassan (Evergreen), Sophia Mwasikili (Luleburgaz Spor Kulubu, Uturuki), Veneranda Mtamo (Tanzanite), Zena Khamis (Mburahati Queens) na Zena Said (Uzuri Queens).Twiga Stars ilifika hatua hiyo ya pili baada ya kuiondoa Namibia kwa jumla ya magoli 7-2 mapema mwaka huu.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment