Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Nahodha amkabidhi Nchimbi changamoto za Mambo ya Ndani

10th May 2012
Print
Comments
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha

Aliyekuwa  Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, amesema wizara hiyo inakabiliwa  na changamoto mbalimbali zikiwemo suala la wakimbizi, uwingi wa wafungwa magerezani na utengenezwaji wa vitambulisho vya taifa.

Alisema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi ofisi waziri mpya wa wizara hiyo, Dk. Emmanuel Nchimbi, hivyo akamtaka akabiliane na changamoto hizo.

Nahodha alisema wizara hiyo inakabiliwa na changamoto ya kuwarudisha wakimbizi 37,000 wa Burundi waliohifadhiwa nchini.

“Wakimbizi hao walitakiwa kurudishwa nchini kwao tangia Aprili 1, mwaka huu, hivyo ni jukumu la wizara yako kutekeleza kazi hiyo niliyoiachia katikati,” alisema Nahodha. Alisema wakimbizi  67,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) hawatarudishwa kwao kutokana na hali ya amani katika nchi kutokuwa ya kuridhisha.

Aliongeza kuwa msongamano wa wafungwa magerezani ni moja ya changamoto inayoikabili wizara hiyo, na kiliundwa kikosi kazi cha kufatilia kesi zisizokuwa za msingi na kuzifuta kesi hizo ili watuhumiwa waachiwe huru.

“Ni jukumu lako ni kuendeleza kazi tulioiachia katikati ya kuhakikisha msongamano wa wafungwa magerezani unakwisha na kesi zisizokuwa na ushahidi zinafutwa na watuhumiwa wanaachiwa huru,” alisema.

Nahodha ambaye amehamishiwa Wizara ya Ulinzi na JKT, alisema, sula la kutengeneza vitambulisho vya taifa ni moja ya changamoto inayoikabili wizara hiyo na mpaka sasa wafanyakazi wa serikali 290,000 kutoka bara na visiwani wameshaandikishwa, hivyo ni jukumu la wizara hiyo kuendeleza kazi hiyo.

Kwa upande wake Dk. Nchimbi alisema atajitaidi kuzikabili changamoto hizo na kutoa wito kuwa vyombo vya dola viendelee kueshimiwa na umma.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles