Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Walimu wakuu 11 watiwa mbaroni

11th May 2012
Print
Comments
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo

Jeshi la polisi mkoani Kigoma linawashikilia wakuu wa shule za sekondari 11 katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma /Ujiji kwa tuhuma za kudahili wanafunzi 493 kinyemela.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai, alisema wanawashikilia kutokana na amri iliyotolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, kuwa wakamatwe kwa kosa la kuwadahili wanafunzi kinyume cha sheria.

Waliokamatwa ni Hamisi Nkilie wa Shule ya Sekondari Kasingirima ambaye alidahili wanafunzi 154; Gwalugano Gwalulayi 52 Shule ya Sekondari Masanga ambaye alidahili wanafunzi 89; Nathani Boranzize wa Shule ya Sekondari Lubuga  aliyedahili wanafunzi 24; Lukasi Magogwa wa Shule ya Sekondari Mlole aliyedahili wanafunzi 11 na Elisha Zirikana 52 wa Shule ya Sekondari Mwananchi aliyedahili wanafunzi 49.

Wengine ni  Batoromeo Morisi wa Shule ya Sekondari Bulonge aliyedahili wanafunzi sita; Desimoni kumwe Robart wa Shule ya Sekondari Wakulima aliyedahili wanafunzi 19; George Bosko wa Shule ya Sekondari ya Katubuka aliyedahili wanafunzi 19; Paulo Lusale  wa Shule ya Sekondari Buteko aliyedahili wanafunzi wanne; Baraka Magambo wa Shule ya Sekondari Rusimbi aliyedahili wanafunzi sita na Costantino Nali wa Shule ya Sekondari Kitongoni alidahili wanafunzi 16.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles