Tuesday May 3, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

TRA kukusanya Trilioni 8.9

19th March 2012
Print
Comments
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekusudia kukusanya kiasi cha  shilingi trilioni 8.9 katika mwaka mpya wa fedha 2012/2013.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Yeremiah Mbaghi wa Idara ya Elimu ya Huduma kwa mlipa kodi alipokuwa akizungumza katika mkutano wa taasisi za udhibiti,wauzaji na wanunuzi ulioandaliwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO), kwa ajili ya kutoa elimu kwa wajasiriamali.

Mbaghi alisema ili serikali iweze kufikia malengo hayo ya ukusanyaji kodi, wajasiriamali hao wanapaswa kulipa kodi stahiki katika biashara zao kwa kuwa bajeti ya serikali hutegemea ukusanyaji wa kodi hizo.

Alisema kwa sasa Mamlaka hiyo  imepanua wigo wake katika ukusanyaji kodi na kuziba mianya ambayo kwa baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu walikuwa wakitumia kukwepa kulipa kodi hasa kwenye maeneo ya mipakani.

Aidha, alisema wameimarisha doria katika mipaka mbalimbali ya nchi kwa ajili ya wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa nje ya nchi kama Kongo na  nyinginezo.

Akitoa mada katika mkutano huo ulioshirikisha wafanyabiasha 45 wa chini na wa kati, Mwakilishi kutoka maduka ya Shoprite Irine Mbonea  aliwashauri wafanyabiashara hao hasa wasindikaji, kuuza bidhaa zao katika maduka hayo.

"Njoo muuze bidhaa zenu katika maduka yetu ya Shoprite tutazipokea ila chakufanya mjitahidi kuongeza ubora katika bidhaa zenu,"alisema Mbonea.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles