Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Maandalizi ya Saba Saba yaanza

12th June 2012
Print
Comments
Kaimu Mkurugenzi Ukuzaji Masoko na Huduma za Biashara ya Nje wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Masha Hussein

Maandalizi ya  Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam Saba Saba yameanza kwa mabanda mbalimbali kufanyiwa usafi ikiwa ni pamoja na kupakwa rangi.

NIPASHE jana ilishuhudia mafundi mbalimbali wakiwa katika maandalizi hayo huku wakifanya usafi kabla ya kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu.

Kaimu Mkurugenzi Ukuzaji Masoko na Huduma za Biashara ya Nje wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Masha Hussein, aliliambia NIPASHE kwamba kwa sasa wanaanda taarifa rasmi kwa vyombo vya habari kuelezea maandalizi yatakuwaje, viingilio,pamoja na makampuni na nchi zitakazoshiriki mwaka huu.

“Nitaandaa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari itayoelezea jinsi maonyesho yatakavyokuwa ili kujua viingilio vitakuwa kiasi gani, makampuni yatakayoshiriki pamoja na mgeni rasmi tunayemtarajia,” alisema Hussein.

Aidha, Hussein alisema kipindi hiki walikuwa na shughuli nyingi kwa kuwa bodi iliyoko sasa ni mpya, hivyo anaiandalia taarifa ya utendaji ndio maana wamechelewa kutoa taarifa.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment