Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

CWT yawa bubu kuhusu walimu kugomea Mei Mosi

1st May 2012
Print
Comments
Rais wa CWT, Gratian Mukoba

Baadhi ya walimu wa shule za msingi na Sekondari za jijini Dar es Salaam, wametishia kugoma kushiriki kwenye sherehe za Wafanyakazi Duniani zinazofanyika leo kwa madai ya kutotekelezwa kwa madai yao mbalimbali, huku Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kikishindwa kutoa tamko.

Wakizungumza na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam kwa masharti ya kutoandikwa majina yao kwenye gazeti, walimu hao walisema kuwa wamechoshwa kutumiwa kila mwaka, huku wakiwa wanaidai serikali malipo yao mbalimbali kwa muda mrefu sasa huku serikali ikiwa inawazungusha.

“Hatutashiriki kwenye sherehe za siku ya wafanyakazi kwani tunaona kama vile tunapuuzwa, umuhimu wetu umekuwa ukionekana kwenye sherehe au shughuli kama hizi tu, wakati tuna madai yetu mbalimbali tunayodai lakini tumekuwa tunazungushwa tu,” alisema mwalimu mmoja.

Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alishindwa kuthibitisha madai hayo pale alipotafutwa na NIPASHE, na alijibu kwa simu kupitia ujumbe mfupi wa maneno kuwa yupo safarini.

“Mimi nipo Tanga, sijui, ila kesho (leo) itaamua, kama wakijitambua na kuacha kuchukuliwa poa,” alijibu.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles