Monday May 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

JK mgeni rasmi Mei Mosi

25th April 2012
Print
Comments
Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani, ambayo kitaifa mwaka huu itakafanyika mkoani Tanga.

Akizungumza na NIPASHE jana, Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Hezron Kaaya, alisema Rais Kikwete amethibitisha kushiriki  katika maadhimisho hayo ambapo  kauli mbiu yake ni  “mishahara duni, kodi kubwa, mfumuko wa bei ni pigo kwa wafanyakazi”.

Alisema katika maadhimisho hayo kila mkoa utaadhimisha siku hiyo na wanamatumaini serikali itakuwa sikivu kuongeza mishahara ya wafanyakazi kima cha chini kiweze kufikia Sh.315,000.

“Inatakiwa serikali iwe sikivu kwa kuongeza kima cha chini cha mishahara kufikia Shilingi 315,000 na tushafanya mazungumzo na serikali kuhusu hilo,” alisema Kaaya.

Aidha, Kaaya alisema serikali inatakiwa ichukue hatua za kudhibiti mfumuko wa bei kwa kuwa umefanya Watanzania wengi kuwa na maisha magumu.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment