Monday May 2, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mhariri Michezo Mtanzania afariki dunia

12th May 2012
Print
Comments
Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Mtanzania Rachel Mwiligwa

Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Mtanzania Rachel Mwiligwa alifariki dunia jana alfajiri.

Kabla ya mauti kumfika, Rachel alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Nemonia ambapo Jumapili alilazwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya matibabu.

Wakati wa uhai wake, Rachel aliwahi pia kuwa mwandishi wa magazeti ya michezo ya Bingwa na Dimba kabla ya mauti kumfika akiwa katika gazeti la Mtanzania kama mhariri wa michezo.

Rachel anategemewa kuzikwa jijini Dar es Salaam keshokutwa.

Kufuatia kifo hicho, Chama Cha Waandishi wa habari za Michezo nchini (TASWA) kimetuma salamu za pole kwa familia yake na wanahabari wote.

Katika taarifa ya Chama hicho iliyosainiwa na Katibu wake, Amir Mhando imesema kuwa TASWA imeshtushwa taarifa za kifo cha Rachel.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles