Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mtibwa yaivika Simba ubingwa

5th May 2012
Print
Comments
  Kocha Azam akimbia waandishi wa habari
Mtibwa Sugar

Mtibwa Sugar yenye wachezaji 10 uwanjani jana iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam katika mechi ya kitatanishi na kuipa Simba ubingwa wake wa 19 wa ligi kuu ya Bara, bila jasho kwenye Uwanja wa Taifa.

Kipa wa Mtibwa Deogratias Munisi alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kusindikizwa kwa nyekundu na muamuzi Owden Mbaga dakika moja kabla ya muda wa kawaida kumalizika.

Munisi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba alionyeshwa kadi mbili hizo kwa kosa la kupoteza muda timu yake ikiwa inaongoza. 

Kwa matokeo hayo, Azam imepoteza matumaini ya mbali ya kutwaa ubingwa wa Bara endapo Simba ingefungwa na Yanga kesho, na yenyewe kuifunga Mtibwa jana na kuilaza Kagera Sugar pia katika mchezo wa kesho.

Lakini sasa Azam iliyobaki na pointi 53 haitoweza kuifikia Simba yenye pointi 59 kileleni.

Timu hizo zilicheza jana kwenye Uwanja wa Taifa ikiwa ni mechi ya marudio baada ya Kamati ya Nidhamu kubatilisha uamuzi wa Kamati ya Ligi wa kuipa Azam ushindi wa mchezo uliovunjika dakika ya 88 wiki iliyopita.

Kocha wa Azam iliyokuwa ikiwania kubadili uelekeo wa ubingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 kutoka kwa Simba ama Yanga inayomaliza katika nafasi ya tatu, Stewart Hall hakutokea katika mkutano na waanindishi wa habari.

Tom Olaba, mwalimu wa Mtibwa ambayo ni timu ya mwisho kuvunja umwamba wa Simba na Yanga miaka 12 iliyopita alisema timu yake ilistahili kushinda kwasababu ilicheza vizuri na kuibana Azam.
Bao la kwanza la Mtibwa lilifungwa na Awadh Issa katika dakika ya 25 akiunganisha mpira wa kona iliyopigwa na Juma Abdul.

Abdul aliipatia Mtibwa bao la pili kwa shuti kali la mpira wa adhabu ndogo kutoka nje ya eneo la hatari kufuatia faulo aliyochezewa winga Vicent Barnabas, robo saa tangu kuanza kwa kipindi cha pili.

John Bocco aliifungia Azam bao la kufutia machozi na la kwake la 18 msimu huu dakika 10 baadaye hivyo kurejesha matumaini ya Azam kujiweka katika mazingira ya ubingwa wake wa kwanza tangu ipande kucheza ligi kuu miaka mitano iliyopita.

Timu zilianza:
AZAM: Mwadin Hassan, Erasto Nyoni, Wazir Omary, Ibrahim Mwaipopo, Luckson Kakolaki, Agrey Moris, Mrisho Ngassa, Bolow Kipre, John Bocco, Salum Abubakar, Tchetche Kipre.

MTIBWA: Deogratias Munisi, Said Mkopi, Juma Abdy, Salvatory Ntebe, Salum Swedi, Shaban Nditi, Hussein Javu, Babu SEif, Thomas Maurice, Awadh Issa, Vicent Barnabas.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles