Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mpango wa dharura wa Ukimwi wajadiliwa

2nd August 2012
Print
Comments
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk. Fatma Mrisho

Mpango Dharura wa  Rais wa Marekani kwa ajili ya Kupunguza makali ya ukimwi (PEPFAR) jana uliandaa jukwaa kwa ajili ya kujadili mazingira ya mipango ya Ukimwi nchini na kuangalia kumbukumbu ya mkutano wa kimataifa wa Ukimwi uliofanyika wiki uliyopita nchini Marekani.

Akizungumza katika kumbukumbu ya mkutano huo, jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk. Fatma Mrisho,  alielezea adhima ya Tanzania ya kujikita zaidi kuwasaidia wale wenye uhitaji katika programu hiyo ya kupunguza makali ya Ukimwi.

Ili kuifikia lengo hilo, Dk. Mrisho alisema kwamba Tanzania itatumia mfumo wa uwekezaji kama njia ya kutathmini mikakati ya kitaifa, mfumo ambao unafanyiwa kazi na serikali kwa kushirikaina na UNAIDS, PEPFAR, DANIDA na Mfuko wa Kimataifa.

Mratibu Mkazi wa PEPFAR toka ubalozi wa Marekani ambaye alikuwa mmoja wa wawezashaji wa jukwaa hilo, aliuelezea mkakati wa mpango wao unaolenga kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na kizazi kisicho na ukimwi kabisa.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment