Wednesday Feb 10, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Ewura yatangaza bei ya mafuta

7th March 2012
Print
Comments
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura)

Bei za mafuta ya imepanda kwa wastani wa asilimia 6.34 kwa bidhaa zote katika soko la dunia.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), petroli inaongoza kwa kupanda bei kwa zaidi ya asilimia 7. Bei za jumla na rejareja kwa aina zote za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la Februari 1, mwaka huu.

Bei ya rejareja kwa  mafuta ya petroli imeongezeka kwa Sh. 153 kwa lita sawa na asilimia 7.67, Dizeli kwa Sh. 119 kwa lita sawa na asilimia 6.01 wakati mafuta ya taa kwa Sh. 104 kwa lita sawa na asilimia  5.35.

Kutokana na ongezeko hilo kwa sasa petroli itauzwa kwa Sh. 2144, dizeli 2096 na mafuta ya taa 2055 kwa lita kwa bei ya rejareja.

 

Ewura imesema mabadiliko hayo ya bei za mafuta nchini yametokana na thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani. 

 

Thamani ya shilingi ya Tanzania imeshuka kwa asilimia 0.13  ikilinganishwa na thamani ya shilingi katika toleo lililopita.

Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimebadilika ambapo Petroli imeongezeka kwa Sh 152.70 kwa lita sawa na asilimia 7.97 na Dizeli  kwa Sh 118.77 kwa lita  sawa na asilimia 6.24 na Mafuta ya taa kwa Sh. 104.49 kwa lita sawa na asilimia  5.57.

Kabla ya bei hiyo kupanda petroli Sh. 1,991 dizeli 1,977 na mafuta ya taa 1,951

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment