Wednesday May 22, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Mmoja afariki vurugu za Mtwara
Mtu mmoja amefariki dunia katika vurugu zinazoendelea Mkoani Mtwara kupinga gesi kusafirishwa, ambapo pia ofisi kadhaa na nyumba moja zimeharibiwa.

Yanga yaishusha Polisi Dom

23rd April 2012
Print
Comments
Davies Mwape

Davies Mwape ambaye ameshutumiwa kwa muda mrefu kwa kukosa makali katika safu ya ushambuliaji ya Yanga, jana alizinduka na kufunga magoli mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuishusha daraja timu hiyo ya makao makuu ya nchi.

Polisi wenye pointi 19 wamebakisha mechi moja dhidi ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha Mei 5, lakini itakuwa ya kukamilisha ratiba tu kwa sababu hata wakishinda hawezi kuzifikia pointi 23 za walio juu yao, Villa Squad na African Lyon, ambao walitoka sare ya 0-0 kwenye Uwanja wa Chamazi jana.

Ushindi wa Yanga uliowafanya wafikishe pointi 46, umebakisha pumzi kidogo ya matumaini ya kumaliza ndani ya 'Top 2' ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa, lakini jambo hilo litategemea mafanikio ya dua mbaya kwa Azam yenye pointi 50 ishindwe kupata pointi tatu katika mechi zao tatu zilizosalia, huku wao wakilazimika kushinda mechi zote mbili zilizobaki dhidi ya Oljoro ugenini Arusha Jumatano na dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa siku ya kufunga msimu Mei 5.

Azam ambayo leo itaikaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Chamazi inahitaji kushinda leo kujihakikishia kumaliza katika nafasi ya pili kwa sababu Yanga wana uwezo wa kufikisha pointi 52 tu. Mechi nyingine mbili za Azam ambazo zote zitafanyika kwenye uwanja wao wa nyumbani zitakuwa ni dhidi ya Toto African Alhamisi na ya kufungia msimu dhidi ya Kagera Sugar Mei 5.

Simba wanaoongoza wakiwa na pointi 56 wanawakaribisha Moro United kwenye Uwanja wa Taifa leo na wanahitaji ushindi na dua ya kuteleza kwa Azam ile wabebe kombe leo. 

Kwenye Uwanja wa Taifa jana, Mzambia Mwape aliifungia Yanga goli la kuongoza katika dakika ya 20, Idrissa Senga akafunga la pili katika dakika ya 54 na Mwape tena akapiga la tatu katika dakika ya 60. Wageni walipata la kufutia machozi katika dakika ya 76 kwa  shuti la mbali kutoka kwa Ismail Nkama.

Kocha wa Yanga, Mserbia Kostadin Papic, ambaye mkataba wake unamalizika kesho, alisema amefurahia ushindi huo lakini anaonekana mnyonge kwa sababu hajalipwa mshahara wake wa miezi miwili.

Alisema alisema ataondoka nchini Alhamisi na kwamba anatarajia atalipwa haki zaki zote kwani kinyume na hapo atafika hata FIFA kuzisaka.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment