Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mgomo wa wafungwa waendelea

11th May 2012
Print
Comments

Mgomo wa chakula wa wafungwa wa gereza la Lilungu umeingia siku ya pili ambapo Mkuu wa Magereza (RPO) Mkoa wa Mtwara ameingilia kati kujaribu kuumaliza, lakini jitihada zake zimegonga mwamba.

Badala yake, wafungwa hao ambao wamegoma kula kwa nia ya kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa, wamemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani au Naibu wake kwenda kusikiliza matatizo yao.

Taarifa zinaekeza kwamba hali za wafungwa hao ni mbaya na kwamba jana mfungwa mwenye namba 303 Abdul Suna anayedaiwa kuwa na umri mkubwa amezimia kutokana na kukaa muda mrefu bila kula wala kunywa maji.

Wafungwa waliogoma ni wa adhabu ya kifo waliopo  katika gereza hilo mkoani Mtwara. Nia ya mgomo huo ni madai ya chakula, kupinga manyanyaso ya kipigo kutoka kwa askari magereza pamoja na rufaa zao kuchelewa kusikilizwa na hali ya gereza kuwa mbaya.

Wafungwa hao wanamshutumu mkuu wa gereza hilo kwamba amekuwa akisimamia ukatili dhidi yao. Walisema tangu Desemba mwaka jana, wafungwa hawapewi matunda, hawapikiwi nyama wala hawawekewi sukari kwenye uji badala yake wanakunywa uji wa chumvi.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles