Tuesday Jun 18, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Walimu 150 waandaliwa kwa sense ya watu

2nd June 2012
Print
Comments
Dk. Hajjat Amina Mrisho

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema kuwa walimu 150,000 wameandaliwa kwa ajili kufanya zoezi la sensa ya watu na makazi litakaloanza Agosti, mwaka huu.

Kamishina wa sensa hiyo, Dk. Hajjat Amina Mrisho, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na wakuu wa vyombo vya habari kwa ajili ya kujadili jinsi watakavyovitumia vyombo vya habari katika kuielimisha jamii juu ya zoezi hilo.

Dk. Mrisho alisema kuwa Serikali imejipanga kuweka idadi yakutosha katika zoezi hilo na kwamba wanategemea kulimaliza kwa kipindi kisichozidi siku tatu.

Alisema wamewachukua walimu wa Serikali na wa shule za binafsi na kwamba kila mmoja atapangiwa kuendana na eneo lake la kazi haitaruhusiwa mtu kuhamishwa eneo lake la kazi na kupelekwa sehemu nyingine kwa ajili ya kufanya zoezi hilo.

Alisema tangu mwaka jana wametoa elimu kwa wananchi ili waweze kuwa na uelewa wa kutosha juu ya sensa kutambua changamoto mbalimbali kupitia zoezi hilo.

Alisema wameandaa maswali ambayo wananchi wataweza kuyajibu kwa umakini na kwamba siku ya tukio kila mmoja atatakiwa kuwa nyumbani kwake ili aweze kuhesabiwa.

Dk. Mrisho alisema kwa wale ambao watakuwa wamelala hotelini watawafanyia sensa kwa kuwa  wameshafanya mazungumzo na wamiliki wa hoteli ili wawajulishe wateja wao kuhusiana na zoezi hilo.

“Tumejipanga vizuri kwani wenye mahoteli tumeshawajulisha ili waweze kutoa elimu kwa wateja wao ifikapo tarehe hiyo na hata maeneo ya vijijini tumejipanga kuwafikia wananchi wote na tumeamua kuwachagua walimu kwa kuwa tayari wanauzoefu,” alisema

Alisema hivi karibuni wanatarajia kutoa semina kwa walimu hao ili wawe na uelewa wa kutosha katika zoezi hilo ikiwemo katika matumizi ya lugha.

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment