Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mahakimu wakwamisha hukumu ya kina Maranda

18th May 2012
Print
Comments
Wafanyabiashara wawili, Farijala Hussein kushoto na Rajabu Maranda

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, jana ilishindwa kutoa hukumu ya kesi ya inayowakabili wafanyabiashara wawili, Farijala Hussein na Rajabu Maranda  ya  kula njama, kughushi na wizi wa Sh. Bilioni  2.266 za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) baada ya mahakimu wawili kuugua.

Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Mkazi Katalina Revocat aliyepo kwenye jopo linalosikiliza kesi hiyo, alisema mahakimu wawili wamepata maradhi, hivyo hukumu hiyo haitasomwa hadi  Juni 26, mwaka huu.

“Jopo halijakamilika kwa sababu mahakimu wengine wamepata maradhi hivyo itasomwa Juni 26 mwaka huu na washtakiwa warudishwe gerezani” alisema Hakimu Revocat.

Mbali na Revocat, mahakimu wengine ni, Fatuma Masengi ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania, aliyepewa kibali na Jaji Mkuu kusikiliza kesi hiyo na Projestus Kahyoza.

Awali, shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Noel Shani, aliifafanulia mahakama hiyo kwamba wamiliki halali wa jina la biashara la Kampuni ya Money Planers & Consultant ni Paul Nyingo na Fundi Kitunga.

Shani ambaye ni Msajili Msaidizi kutoka Wakala wa Majina ya Biashara (Brela), alidai kuwa, washtakiwa Maranda na Hussein sio wamiliki halali wa jina hilo la biashara.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kuwa, Machi 20 na Desemba 25, mwaka 2005, walijipatia ingizo la Sh. 2,266,049,041.25 wakidai kwamba Kampuni ya B. Graciel ya Ujerumani imehamishiwa deni na Kampuni ya Money Planers & Consultant ya Tanzania.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment