Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mkutano mkuu Yanga Julai 15

12th May 2012
Print
Comments
Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga

Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, amesema mkutano mkuu wa klabu hiyo umepangwa kufanyika Julai 15 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nchunga alisema kuwa kamati ya utendaji ya klabu hiyo imekubaliana mkutano mkuu wa klabu hiyo kufanyika Julai 15 kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo.

"Hivyo nawaomba wanachama wa klabu hii kuhakikisha wanalipia ada za kadi zao ili kujihakikishia kushiriki kwenye mkutano huu wa klabu yetu," alisema.

"Mwanachama ambaye atakuwa hajalipia kadi yake hatoruhusiwa kuingia kwenye mkutano."

Nchunga amekuwa katika shinikizo kubwa la wanachama, wakiongozwa na baadhi ya wazeee wa klabu hiyo, la kuitisha mkutano wa wanachama ambao haujafanyika tangu aingie madarakani karibu miaka miwili iliyopita.

Lakini wanachama hao pia wamemtaka mwenyekiti huyo kujizulu kutoka nafasi hiyo mapema kufuatia timu kufanya vibaya na kushika nafasi ya tatu kwa mara ya kwanza tangu 1988.

Katika kuzuia shinikizo hilo la kujiuzulu, Nchunga aliiambia Nipashe wiki iliyopita kuwa angeitisha mkutano huo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ligi.

Nchunga amewataka wanachama wa klabu hiyo kuwa watulivu katika kipindi hiki na kusubiri mkutano mkuu ambapo kila mwanachama atakuwa na nafasi ya kutoa maoni yake.

"Kama mtu ana mawazo yake basi asubiri mkutano mkuu aje aweke mambo wazi kuliko sasa hivi kueneza uongo na chuki ambazo hazina faida yoyote kwa klabu yetu," alisema Nchunga.

Alisema kama kuna mwanachama hautaki uongozi uliiopo madarakani wasubiri siku ya mkutano mkuu na kueleza hoja zao na kwa sasa waache kueneza maneno ya chuki.

Mkutano huo wa Nchunga na wanahabari ulifanyika huku nje ya ukumbi vurugu kubwa zikiendelea.

Vurugu hizo zilikuwa kati ya wanachama wanaotaka Nchunga ajiuzulu ambao walikuwa wakitaka kuingia kwenye mkutano huo kwa lengo la kuuvunja lakini wakazuiwa na wanachama wanaomuunga mkono Nchung, pamoja na polisi waliokuwepo klabuni hapo jana kulinda amani.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles