Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Simba, Yanga sasa kuvaana J`pili

4th May 2012
Print
Comments
Timu ya Yanga

Watani wa jadi Simba na Yanga sasa watakutana keshokutwa Jumapili ikiwa ni katika mechi ya funga dimba ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa mwaka 2011/ 2012 badala ya kesho Jumamosi kama ilivyokuwa inajulikana kwenye ratiba yake ya awali.

Mabadiliko hayo yametokana na maamuzi yaliyofanywa juzi na Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ambayo iliamua mechi namba 162 ya ligi hiyo kati ya Azam na Mtibwa Sugar ambayo ilivunjika dakika za lala salama irudiwe leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika kujiandaa na mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani Simba iko Zanzibar ikijinoa wakati wapinzani wao Yanga wenyewe wako Bagamoyo mkoani Pwani.

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema jana kuwa tayari klabu zote zimeshajulishwa kuhusiana na mabadiliko hayo na hiyo imetokana na kuzipa Azam na Mtibwa mapumziko ya saa 48 kama kanuni za ligi zinavyoeleza.

Osiah alisema kuwa shirikisho linaamini mechi zote za mwisho zitamalizika katika hali ya amani hatimaye bingwa wa ligi ataweza kupatikana.

Alisema kuwa jana jioni Kamati ya Ligi ilitarajiwa kukutana kufanya maandalizi ya mechi hizo ikiwemo kuthibitisha majina ya waamuzi ambao watachezesha michezo hiyo.

Mbali na mechi hiyo ya watani, Jumapili pia Azam itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wake wa Chamazi, JKT Oljoro wakiivaa Polisi Dodoma jijini Arusha huku Ruvu Shooting wakiwa wenyeji wa Villa Squad kwenye Uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.

Coastal Union iliyo chini ya Jamhuri Kihwelu 'Julio' itacheza na Toto African kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, African Lyon ikichuana na JKT Ruvu huko Manungu Turiani na Moro United ikimaliza na Mtibwa Sugar Jamhuri mkoani Morogoro.

Timu za Polisi Dodoma na Moro United tayari zimeshashuka Daraja huku ikisubiriwa nyingine moja kuungana nao.

Polisi Morogoro, Prisons ya Mbeya na Mgambo Shooting ya Tanga ndio zimepanda daraja na msimu ujao zitacheza Ligi Kuu ya Bara.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles