Tuesday Feb 9, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Tovuti ya Sekreterieti ya Ajira yazinduliwa

26th April 2012
Print
Comments
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, imeitaka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kutoa ajira bila upendeleo wakati idara mbalimbali za serikali zinapotangaza nafasi za kazi ili kupata watumishi wenye sifa serikalini.

Waziri Ghasia aliyasema hayo Jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akizindua Tovuti ya Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma inayojulikana kwa www.ajira go.tz

Alisema Sekretarieti hiyo sasa inatakiwa kuachana na mazoea ya kutoa ajira kwa kuendekeza ukabila na matokeo yake wanajikuta wanatoa ajira kwa watumishi wasiokuwa na sifa na kushindwa kukidhi malengo ya serikali.

Aidha, alitaka Sekretarieti hiyo kutumia tovuti hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali zinazohusiana na mchakato wa kutangaza nafasi za kazi, kusaili waombaji wenye sifa na kuwapangia vituo vya kazi kwa watakaokuwa wamefaulu.

Mwenyekiti wa Sekretarieti hiyo, Bakari Mahiza, alisema suala la kuwa na watumishi wenye sifa na ujuzi wa kutosha katika utumishi wa umma ni muhimu katika dunia ya leo ambapo kuna ushindani mkubwa wa kimaendeleo na kiteknolojia.


SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment